Quantcast
Channel: Dar city center » News
Viewing all 39 articles
Browse latest View live

Kalapina afungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya Ubunge wa Kinondoni

$
0
0

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Kalama Masoud aka Kala Pina amefungua kesi mahakamani ya kupinga matokeo hayo.

3X6A6470

“Kiukweli matokeo yale ya Jimbo la Kinondoni sikubaliano nayo kutokana na mapungufu ambayo yalikuwa yamejitokeza katika uchaguzi… kulikuwa na mapungufu mengi ikiwemo kutishwa kwa mawakala wangu katika kata ya Tandale kilichopelekea baadhi ya mawakala wangu kuondoka na wengi walikuwa akina mama”  ameimbia Millard ayo

“Nimeazimia kuupinga uchaguzi huu kwa kwenda Mahakamani kwa sababu naona Demokrasia haikutumika ipasavyo na iliminywa… kuna baadhi ya maeneo watu wanalalamika wamekimbilia Mahakamani kutokana na matokeo yasiyo sahihi, na mimi mwenyewe natarajia kwenda kusikiliza hii kesi Mahakamani wiki ijayo” Aliongeza Kla pina

Source: Millardayo.com

 


Exclusive Video: Mrembo ‘Dati’ azungumzia kilakitu mpaka mahusiano yake!

$
0
0

Dati ni mmoja kati ya mabinti wenye mvuto ambao wamefanya kazi nzuri kwenye muziki wa kizazi kipya yaani Bongo Fleva 2015. Msanii huyu alizaliwa Tanzania na kukulia Sweden ambako wazazi wake wanaishi, hadi hii leo, mihangaiko ya muziki wake ilianzia Nchini Jamaica then alirejea nyumbani kwao Sweden.

Hata hivyo tangu akiwa na miezi 6 hakuwahi kanyaga tena Tanzania lakini kwa usemi wetu wa mkataa kwao ni mtumwa 2015 ‘Dati’ ameweza kurejea mahali alipozaliwa yaani Tanzania na kuachia Exclusive official Video ya wimbo wa “Can Do” amewatumia ma-director wa hapa hapa kwetu Tz, Khalfan, Hanscana & CBH.

Zilipo salia siku mbili za mrembo huyo kukaa hapa Tz Team yetu ilimtafuta na kufanyanaye Exclusive Interview ya mwisho mwisho, coz Ijumaa ndio siku ambayo aliondoka kwenda Sweden. Katika hiyo Interview Dati amezungumzia vitu vingi ikiwa ni pamoja na tofauti aliyopo kwenye muziki wa Tanzania & Swiden, changamoto, mafanikio, malengo yake, Life style yake, pia Mahusiano yake ya kimapenzi.

Hivyo basi ukiwa kama shabiki wa burudani ya muziki na habari za wasanii wanao fanya poa tumia dakika zako kadhaa kuitazama hii video interview hapa ukimaliza tunakuomba usibanduke kwenye tovuti yetu kwania bado tunaendelea kukujuza zaidi. Enjoy with us

LADY IN RED KUFANYIKA TANZANIA NA UK! 2016

$
0
0

Miongoni kati ya Burudani Duniani ni pamoja na “Fashion Industry’ yaani mitupio inayowafanya watu kuwa katika good appearance Wanawake kwa Wanaume kuanzia miguuni mpaka kichwani. Wanamitindo kutoka hapa nchini Tanzania wamekuwa na utaratibu wa kuandaa Fashion Show ambazo zinatoa opportunity kwa Designers na Models.

Hivyo basi new update kutoka Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous ambaye kila mwaka huandaa Fashion Show inayo wakutanisha Designers “Lady in Red” amesema kuwa “Mwezi huu nitahakikisha “Lady in Red” inafanyika Tanzania coz tarehe 17 January, 2016, nategemea kukutana na designers pale Regency Hotel Mikocheni saa 10:00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya “Lady in Red” inayotegemea kufanyika 31/1/2016 katika ukumbi wa “Danken House’

Pia Asya  Idorous aliongeza kuwa “2016  “Lady in Red” itaifanyika Tanzania na United_Kingdom (UK) . So kwa wale wapenzi wa mitindo hapa ndio pake staytuned yaani kitu ni “Lady in Red” Cheers 2016.

12510229_1090788364288759_5261505416818263081_n

KAMATI YA MISS TANZANIA YA KINA JOKATE YAJIVUA UONGOZI!

$
0
0

Kamati ya Miss Tanzania ya kina Jokate Mwegelo na Juma Pinto iliyoteuliwa na Kampuni ya Rhino Agency imejiondoa madarakani, kufuatia tofauti zilizo ibuka baina yao, wajumbe wa kamati hiyo wamebainisha haya wakati walipokutana na waandishi wa habari jana  na kufafanua zaidi kuhusiana na taarifa hiyo.

Miongoni mwa sababu zilizo sababisha Kamati hiyo kung’oka madarakani ni pamoja Kampuni ya “Rhino Agency”  kuingilia Majukumu ya Kamati hiyo.

RAPPER WAKAZI KUTOKA TANZANIA AWANIA “KORA AWARDS” NAMIBIA

$
0
0

Rapper Wakazi kutoka hapa home Tz ambaye ni mkali kwenye anga za muziki wa Hip Hop ameingia kwenye Kinyang’anyiro cha kuwania tuzo “Kora_Awards ” ya Best Hip Hop Act 2016,  Tuzo ambazo zinategemea kutolewa March 20th huko Windhoek, Namibia.

Best Hip Hop Act 2016, Awards Nominees

Sarkodie (Ghana)
Stanley Enow (Cameron)
KO (South Africa)
Kiff No Beat (Ivory Coast)
Hamzaoui Med Amine (Tunisia)
Wakazi (Tanzania)

Hata hivyo kutoka Tanzania hatakuwa pekeyake bali, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Yamoto Band na Mrisho Mpoto, pia ni wasanii ambao wanawania tuzo siku hiyo.

Kuhusiana na ushidi Rapper “Wakazi” amesema kuwa  “Kuwa nominated tayari kwangu ni ushindi tosha!! Nimekuwa nafanya Muziki officially kwa kama 4 years now na sijawahi kuwa nominated Tuzo yoyote ile hata mara Moja. So nomination hii ina maana kubwa sana kwangu na ukichukulia pia ni Tuzo Za kimataifa. Nikishinda nitafurahi ila haimaanishi kuwa nitakasirika nisiposhinda. Coz kuchaguliwa kwangu naweza kusema ni kutokana na ubora wa Kazi zangu, consistency Pamoja na support Ya mashabiki ambayo ndio iliyoweza kufanya nionekane.”

Hivyo kwa wadau wa muziki make sure that unaonesha support yako ya kutosha ili kuhakikisha  Rapper “Wakazi” anaibuka mshindi na kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia Muziki wetu wa Hip Hop. Umoja ni nguvu, Utengani ni udhaifu. Ili ashinde Please Send “Kora 123″ to +248984000 to vote for Wakazi (@Wakazimusic) as the #BestHipHopAct in 2016 @Kora_Awards.  Cheers 2016.

TEAM YA MAANDALIZI YA “LADY IN REDY 2016″ YAKUTANA NA WANAHABARI LEO DANKEN HOUSE

$
0
0

Team ya maandalizi ya Fashion Show maarufu kama “Lady In Red 2016″imekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa “Danken House” kujadili na kutoa hamasa kwa Designers na wadau mbalimbalia ambao pia ni wapenzi wa mitindo.

Uongozi huo ambao unasimamiwa na Mama wa Mitindo ambaye anajulikana kama “Asya Idarous”  umesema kuwa “Jukwaa la “Lady In Red 2016″ litakuwa la ainayake kufuatia jitihada na juhudi zinazofanywa na walengwa wa tukio hilo, ambalo linategemea kupandisha Designers wengi zaidi hapa nchini siku ya Jumapili 31/1/2016 katika ukumbi wa Danken House.

Miongoni kati ya Designers watakao panda kwenye Stage siku hiyo ni Bemy Masai, Kelly Peter, Faustin Simon, Mtetesi Forcus, Barnabas, Mwanahamisis Kiroho, Nelson Thomas, Walter Demarian, Dorine Lymo, Evemary Sospeter, Fatma Rashid, Samweli Zebedayo, Kulwa Mkwandule, Jocktan Makeke, Saleem Siwila, Love Delamo, Abdul Mwene, Karol Mngumbi Jay Julius, Furaha, Joshua, Benja, Lili, Veronica, Rukia Walele nk.

Hivyo kama nawewe ni mpenzi wa mitindo usikubali kupitwa na tukio hilo, kiingilio ni buku 10000/= na viti vya mbele ni 30000/= Nyote mnakaribishwa ulisema oungozi wa maandalizi ya Tukio hilo.

 

(Picha na Maelezo by Victor Petro from Teamtz)

DSCN9613 DSCN9616 DSCN9618 DSCN9620 DSCN9621 DSCN9622 DSCN9623 DSCN9624 DSCN9625 DSCN9650 DSCN9652 DSCN9656 DSCN9657

Picha za Pamoja za Designers mara baada ya kumaliza mazungumzo ya “Lady In Red 2016″ na waandishi wa Habari leo.

 

Rosse Ndauka atimiza ndoto yake leo “Rozzie Magazine”

$
0
0

Tukiwa tunaumalizia mwezi wa kwanza 2016, Mwigizaji wa Filamu za kibongo maarufu kwa jina la Rosse Ndauka Leo ametimiza ndoto yake mara baada ya kuzindua Magazine yake ambayo inaitwa “Rozzie Magazine” iliyokuwa online na hatmaye sasa inapatikana kwa Hard Copy, baada ya tukio hilo la kipee katika maisha ya Rosse leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe huu hapa huku akiwa ameambatanisha na picha unayoiona hapa.

“Namshukuru Mungu kwa yote, ilikua ndoto yangu kubwa kuileta Rozzie Magazine iwe kwenye Hard Copy baada ya kuwa online kwa muda mrefu, Leo hii nimezindua Rozzie Magazine ambayo sasa mtaweza kuipata mitaani, kwa sasa itakua free na itapatikana sehemu mbali mbali.

Thanks to my team and everybody who was there from the scratch.. Niwashukuru na Nyie mashabiki wangu hope mtaendeleza support kwa hili linalokuja. I prayed 2016 to be a year of success,God is listening… Papah Ahsante! 😘”

Exclusive Audio: Kauli ya Nay Wa mitego kuhusu kuiponda Bongo muvi + Ray

$
0
0

Baada ya gumzo mtandaoni la msanii wa Hip Hop maarufu kama “Nay wa mitego” kutapakaa kuhusiana na kuiponda Tasnia ya Bongo Movi + Vincent Kigosi a.k.a Ray siku chache tu zilizopita kupitia misitari iliyopo ndania ya Track hiyo mpya ambayo bado haijatoka imepewa jina la”Shika Adabu yako”.  Hapa Teamtz inakuletea Exclusive kutoka kwa “Nay Wa mitego”  dakika chache tu! zilizo pita.

“Kiukweli nikwamba ngoma ipo na kesho Tarehe 9 natoa hiyo ngoma kama nilivyo sema awali kuwa mwaka huu nitakuwa natoa ngoma zangu Tarehe 9,6,19,16,29,26, So walioanza kupaniki before sijui kama hawakusikia kilichomo ndani lakini kunamengi zaidi.

Ngoma inatoka kesho sijui nini kitatokea, sinamengi ya kuongea nafikiri wenye kupambana watapambana lakiki mimi naongea ukweli, coz muziki wa Hip Hop unamruhusu mtu kufanya kitu kwa ajili ya kurekebisha, mimi nimeonge vitu ambavyo vipo sio ugomvi lakini atakaye taka ugomvi tutaona nini kitatokea.

Lengo langu kubwa la kutunga ngoma hiyo ni kuweka vitu sawa coz kuna vitu vimelala kunatakiwa kuwe na amsha amsha, ndio kidogo kunachangamka, kuna mambo yamekaa kaa tu hayaeleweki, nimeongea vitu vingi sana. Mwaka huu nitakuwa na speed ya tofauti kidogo nadhani kwa mashabiki wangu wata-enjoy, ku-relax na kujivunia.”  Nay Wa mitego


New: B-Gway ft Mesen Selekta – Mpera Mpera ( Official Video )

$
0
0

Rapper B Gway ameachia video yake mpya wimbo unaitwa “Mpera Mpera” ft. Mesen Selekta, tumia dakika zako kadhaa kuitazama hapa ukimaliza tunakuomba uendelee ku-enjoy nasi coz bado tunaendelea kukujuza zaidi. 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akiri Gongo kutengenezwa kwa kutumia Kivyesi

$
0
0

Ni taarifa ambayo kwa upande mwingine inasikitisha kufuatia namna ambavyo operation ya kuwasaka wanao tengeneza pombe aina ya Gongo huko wilaya ya Rombo. Kwa mujibu wa  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makala amekiri kuwa ni kweli wilaya ya Rombo ulevi wa pombe ya Gongo umekithiri.

“Kuna aina ya vitu ambavyo wanatumia kutengeneza hizo Gongo wanatumia Mbolea ya Urea wanatumia Battery, pia wanatumia vivyesi vya binadamu.”  Zaidi msikilize hapa

New: Nay Wa Mitego –“Shika Adabu yako” ({Audio}

$
0
0

Ile ngoma ya Nay Wa mitego ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu ambayo msanii huyo kawaponda Bongo Movi + Vincent Kigosi (Ray), Wema Sepetu, Ommy Dimpoz, Shetta, Dj Choka, BASATA, nk. kupitia mshairi ya ngoma hiyo “Shika Adabuyako” inapatikana hapa.  Tumia dakika zako kadhaa kuisikiliza hapa ukimaliza stay on kwenye website yetu coz bado tunaendelea kukujuza zaidi.

Ommy Dimpoz ajibu mashambulizi ya Nay Wa Mitego

$
0
0

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva maarufu kama Ommy Dimpoz amejibu mashambulizi baada ya kupondwa na Rapper Nay Wa Mitego kwenye ngoma yake mpya ambayo imetoka jana tarehe 9, Track inaitwa “Shika Adabuyako” kwenye ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz amemjibu Nay kama ifuatavyo:

“Barua ya wazi kwa Neema wa Mitego kwanza pole kwa Malezi ya Watoto ambao mama zao wamekukimbia, hakuna Mwanamke ambae anaweza kuishi na mwanaume mwenye tabia za kike kama zako inatakiwa ujiulize una tatizo gani maana km umaarufu mavi unao,nyumba unayo,magari unayo na hivyo ndo vitu dada zetu wanapenda lakini kwanini wanakukimbia pili kila nikiwaangalia watoto naona kabisa hamjafanana kuna umuhimu wa DNA Da Neema trust me.

Hiyo video nimekuwekea hapo juu ni kukuonyesha kuwa mimi na wewe Ligi zetu hazifanani vitu navyokula mimi wewe utaishia kuviona kwenye TV maana kuvipata mpaka uwe Unapanda sana Ndege sasa mimi najaza passport ya Tatu wakati wewe hata kurasa 4 za passport yako ya kwanza hujamaliza Sasa wewe ushazoea wanawake zako wa jumuiya basi unataka kila mtu apost demu wake haya sasa Chuma hiko kimetoka ulaya kuja kufuata dodoki nimekujibu ili nikusaidie promo ya nyimbo yako Atleast upige na Vishoo baba Sema nakuomba usirushe ngumi tu maana nakujua Mzee wa Kupanic Maana katika hao mabebi mama wako kuna mmoja nilishapitaga nae Uliza vizuri atakwambia kama jogoo anawika au vipi Ukitaka kudownload wimbo wa@naytrueboy #ShikaAdabuYako nenda kwenye bio ya Da Neema” Hayo ni majibu ya Ommy Dimpoz kwa Nay

ommy 2

VIDEO: ASYA IDAROUS NA RICH MAVOKO WATUA LONDON

$
0
0

Mama wa mitindo Asya Idarous khamsin aa Rich Mavoko watua London kwa ajili ya maandalizi ya usiku wa lady in red London, Onesho  la mavazi kwa ajili ya Valentine, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Rich Mavoko na waimbaji kibao Dress code ni red and white.  Itakuwa ni usiku wa Tarehe 13/Feb/2016  Venue ni starlight suite London Tiket zinauzwa Na mlangoni zitakuwapo. Asya na Rich Mavoko wamealikwa na  CLUBMALIBU London. Yatakayo jili tutakujulisha endelea kuwa pamoja nasi.

 

Tamko la BASATA Kuhusu wimbo wa Nay Wa mitego –“Shika adabu yako”

$
0
0

BASATA imetoa kauli hiyo kupitia Katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo Godfrey Lebejo, alipokuwa akiongea katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba anaamini hata kwenye media wimbo huo hautapigwa.

“Ni wimbo ambao haufai na ni msanii ambaye I dont know hata unashindwa kumpima ana akli ya namna gani, au kwa nini ameamua kufanya hivyo, lakini watu kama hao kwenye jamii wapo, ni kazi ambayo haifai katika jamii kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”, alisema Godfrey.

Katibu huyo wa BASATA amesema kinachotakiwa kwa Ney ni kujitambua kama yeye ni kioo cha jamii, na kwa kufanya vitendo kama hivyo si sahihi kwake kwani jamii inamtazama yeye.

“Anachofanya afikirie yeye ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii, kwa sababu mtu anayefanya namna hii asidhani kama anamdhalilisha mtu, anajidhalilisha yeye mwenyewe kwa sababu mtu yeyote ambaye anatoa lugha chafu, anafanya vitendo vya aibu, asidhani kama anamdhalilisha mtu, kwa hiyo yeye mwenyewe ni kama hayawani fulani tu”, alisema Godfrey Lebejo.

Audio: Dudu Baya aahidi kumshushia kipigo Shetta kama Mr.Nice

$
0
0

Mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania maarufu kwa jina la  “Dudu Baya” ambaye aliwahi kutamba na ngoma zake kibao ikiwa ni pamoja na wimbo wa  “Mpenzi”. Dudu Baya ambaye ni CEO wa Mambaz Ent, Mambaz Group Limited(M.G.l) Exclusive amewasiliana Teamtz na kuzungumzia vikali kuhusiana na jinsi ambavyo atamshushia kichapo  Hit wa ngoma ya “Shikorobo” maarufu kama Shetta.

Sakata hilo limeibuka mara baada ya Shetta kujitangaza kuwa yeye ni Mamba, kwenye Media pasipo kujali kuwa hilo jina  Dudu Baya huwa analitumia tangu muda mrefu kama a.k.a yake.

Hivyo Dudu Baya ametoa tamko la kumuonya “Shetta” kama mjukuu wake kwenye Game la Muziki, hapa nchini, amesema kuwa ili ajiepushie Matatizo inabidi aombe msamaha na kuweka wazi kuwa hata tumia tena jina la “Mamba” la sivyo akileta kiburi kitakacho fuata, Dudu baya atakumbushia enzi za Mr. Nice kwa kumshushia kichapo kizito. Kama atakimbilia Mahakamani Dudu Baya amesema yupo fiti na wanasheria wake Maana hata kwa Mr. Nice amesema ilikuwa hivyo hivyo. Tumia dakika zako kadhaa kusikiliza alicho kisema Dudu baya hapa.


Rapper Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka, amefariki dunia

$
0
0

Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka, amefariki dunia alfajiri ya Jumanne hii.

20160215213132

Woka amefariki baada ya juzi kupata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo. Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Sikiliza Kipande cha Wimbo mpya wa Belle 9 –“Without You” hapa

$
0
0

Kipande cha Wimbo mpya wa msanii Belle 9 – “Without You” kilicho vuja mtandaoni kinapatika hapa, hivyo kama ulikuwa bado huja kisikia tumia time hii kidogo ku-enjoy with us hapa, then endelea kutembelea tovuti yetu kwani bado tunamengi ya kukujuza zaidi.

LADY IN RED 2016 AFTER PARTY KUFANYKA KESHO JUMAMOSI

$
0
0

Baada ya mama wa mitindo Maarufu kama Asya Idarous kwenda kuiwakilisha Tanzania kupitia Tasnia hiyo nchini London kwa kufnya Onesho la Lady In Red 2016 siku ya Tarehe 13/2/2016, iliyo pambwa kimuziki  na Nyota wa Bongo Fleva Rich Mavoko kwa udhamini wa ClubMalibu London,  Kesho Jumamosi Tarehe 20/2/2016 After Party ya Lady In Red 2016 itafanyika Regecy Park Hotel mikocheni Jijini Dar.

Katika Party hiyo kutakuwa na designers pamoja na  wadau wengine wa mitindo, Designers wote walio shiriki Lady In Red 2016 iliyofanyika tarehe 31/1/2016 Tanzania watapewa Certificate za Shukrani.  Party hiyo itaanza ku- shine kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa sita usiku, kumbuka haina kiingilio wapenzi wa mitindo wote wanakaribishwa unakosaje mtaarifu na mwenzio.

Dina Marious amezindua jarida lake la Mtoto.

$
0
0

Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo cha EFM, Dina Marious amezindua jarida lake la Mtoto.

12747583_784281995049068_1116832731_n

Dina akiwa na mtoto wake, Zion Reuben Ndege

Jarida hilo ni maalum kwaajili ya watoto na malezi. Akiongea kwenye uzinduzi ulioambatana na birthday ya miaka miwili ya mtoto wa kiume, Zion, Dina alisema kuwa mtoto huyo ndiye aliyempa hamasa ya kuanzisha jarida hilo.

12751600_682337205202115_478248833_n

Katika toleo la kwanza la Mtoto Magazine, Zion ndiye amekuwa cover story ambapo Dina amesimulia kila hatua ya jinsi alivyojifungua na kubadilisha maisha yake. Kupitia Instagram pia, mtangazaji huyo alifafanua zaidi.

12751107_195728330788227_2008140012_n

“Nilipompata Zion kama mzazi yoyote ilikuwa ni furaha sanaa alileta furaha maishani mwangu na mwanzo mpya katika maisha yangu,” aliandika.

“Katikati maisha yangu yote nilikuwa muoga sanaa kupata mtoto sikuwa najua nitaanzia wapi kumlea. Zile story za wakinamama waliotangulia kuwa kuzaa kunauma zilikuwa zinanipa stress saana. Lakini Nilimuomba Mungu nikifikisha miaka 30 Mungu anijaalie mtoto katika mahusiano yanayoeleweka.Zion hakuwa bahati mbaya siku ambayo baba yake alisema anatamani tupate mtoto Mungu aliweka tiki matamanio hayo wiki iliyofuata nilishika ujauzito.”

12728506_1569850436638911_908962986_n

“Nikiwa natimiza miaka 30 nilikuwa na mimba kubwa ya Zion na nikamzaa nikiwa na miaka 30 nikaamini ni mpango wa Mungu. Nilipopoteza leo tena nilihuzunika sana nikaanza kukufuru Mungu.Kwamba kwa miaka 8 mfululizo nimekilea kipindi leo nimeenda kujifungua narudi nakuta nafasi hiyo haipo kwa nini? Kwa nini kuzaa kubadilishe tena ghafla?

Nakumbuka siku hiyo hata kunyonyesha sikuweza kabisa kabisa Lakini nikamuomba Mungu anipe muongozo anataka kunipeleka wapi? Kwa sababu ya Zion niliweza kuja na product ya mafuta ya nazi Dina Marios Coconut Baby Oil. Alipotimiza mwaka mmoja picha za birthday yake ndio zilileta wazo la kuanzisha magazine ya parenting/malezi .Later nikajoin @efm_93.7 radio nakuanza kipindi kipya cha UHONDO. Nilianza upya na MTOTO wangu Zion ndio inspiration ya mwanzo wangu mpya.

10401864_589055227911914_750500133_n

Baada ya mwaka mmoja kupita wa kulipika wazo jana nikafanikiwa kutambulisha magazine ya MTOTO kwa ndugu,jamaa na marafiki waliokuja katika birthday party ya Zion. Na magazine cover story toleo la kwanza yupo Zion na mimi mama yake kukusimulia mengi maana yeye ndio inspiration ya hiyo magazine. Lolote tunalomuomba Mungu atatupa lakini sio kwa picha ile tunayoitaka ni kwa namna apendavyo yeye na anavyoona inakufaaa. Usikose nakala ya MTOTO magazine kuanzia wiki ijayo kusoma mengi yahusuyo malezi ya watoto wetu . Litauzwa Tsh 5,000 tu!”

Viewing all 39 articles
Browse latest View live